Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarfa zaidi zinasema, kiongozi huyo anaingia rasmi katika orodha ya wagombea wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Hivi karibuni pia Rais wa zamani wa mpito Catherine Samba-Panza, ambaye hana uhusiano na chama chochote cha siasa, ametangaza kuwa, atawania kiti cha urais katika uchaguzi ujao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Catherine Samba-Panza aliteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Januari 2014, ilipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Catherine Samba-Panza, ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika madaraka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati, alitoa nafasi kwa Faustin-Archange Touadéra, mshindi wa uchaguzi wa mwezi Machi 2016.
342/